عَنْ عُمَرَ بْنِ الخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ:
أَنَّ رَجُلًا مِنَ اليَهُودِ قَالَ لَهُ: يَا أَمِيرَ المُؤْمِنِينَ، آيَةٌ فِي كِتَابِكُمْ تَقْرَؤُونَهَا، لَوْ عَلَيْنَا مَعْشَرَ اليَهُودِ نَزَلَتْ لاَتَّخَذْنَا ذَلِكَ اليَوْمَ عِيدًا، قَالَ: أَيُّ آيَةٍ؟ قَالَ: {اليَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الإِسْلاَمَ دِينًا} [المائدة: 3] قَالَ عُمَرُ: قَدْ عَرَفْنَا ذَلِكَ اليَوْمَ، وَالمَكَانَ الَّذِي نَزَلَتْ فِيهِ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَهُوَ قَائِمٌ بِعَرَفَةَ يَوْمَ جُمُعَةٍ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 45]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Omari bin Khattwab -radhi za Allah ziwe juu yake-:
Kuwa mwanume mmoja katika Mayahudi alisema kumwambia: Ewe kiongozi wa waumini, kuna Aya ndani ya kitabu chenu hua mnaisoma, laiti ingelikuwa imeteremka kwetu sisi jamii ya Mayahudi, basi tungeifanya siku hiyo kuwa sikukuu, akasmea: Ni Aya ipi? Akasema: "Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini." [Al-Maaida: 3] Omari akasema: Tunaijua siku hiyo, na mahali ilipoteremka aya hiyo kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa kasimama Arafa siku ya Ijumaa.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 45]
Alikuja mtu mmoja katika Mayahudi kwa kiongozi wa waumini Omari radhi za Allah ziwe juu yake akasema kumwambia: Kuna aya ndani ya kitabu chenu cha Qur'ani mnaisoma, lau ingeliteremka kwetu jamii ya Mayahudi katika kitabu chetu cha Taurati basi tungeifanya siku hiyo kuwa sikukuu kwa kuisherehekea; kwa kushukuru neema ya kuteremka aya hii tukufu, Omari radhi za Allah ziwe juu yake akasema kumwambia: Ni Aya ipi?. Akasema: "Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini." Akasema Omari radhi za Allah ziwe juu yake: Tunaijua siku hiyo, na sehemu iliyoteremka aya hii tukufu, aya hiyo imeteremka siku ya Iddi, nayo ni siku ya Ijumaa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake naye akiwa amesimama Arafa, nazo ni siku mbili tukufu kwa Waislamu.