عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ:
كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدْعُو وَيَقُولُ: «اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ القَبْرِ، وَمِنْ عَذَابِ النَّارِ، وَمِنْ فِتْنَةِ المَحْيَا وَالمَمَاتِ، وَمِنْ فِتْنَةِ المَسِيحِ الدَّجَّالِ».
وفِي لَفْظٍ لِمُسْلِمٍ: «إِذَا فَرَغَ أَحَدُكُمْ مِنَ التَّشَهُّدِ الْآخِرِ، فَلْيَتَعَوَّذْ بِاللهِ مِنْ أَرْبَعٍ: مِنْ عَذَابِ جَهَنَّمَ، وَمِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ، وَمِنْ فِتْنَةِ الْمَحْيَا وَالْمَمَاتِ، وَمِنْ شَرِّ الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1377]
المزيــد ...
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akiomba akisema: "Allaahumma inniy a'udhubika min adhaabil Qabri, wa min adhaabin naari, wamin fitnatil mahyaa wal mamaati, wamin sharri fitnatil masiihiddajjaali" Ewe Mola wangu hakika mimi ninajilinda kwako kutokana na adhabu ya kaburi, na kutokana na adhabu ya moto, na fitina za uhai na za kifo, na kutokana na fitina za masihi dajali".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1377]
Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akiomba kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na mambo manne, baada ya tashahudi ya mwisho na kabla ya swala, na akatuamrisha tuombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na mambo hayo,
Jambo la kwanza: Kuomba kinga kutokana na adhabu za kaburi.
Jambo la pili: Kuomba kinga ya kuepukana na adhabu ya moto siku ya Kiyama.
La tatu: Kuomba kinga itokanayo na fitina za uhai ikiwemo matamanio ya dunia yaliyoharamishwa na ikiwemo pia shub-ha (utata) wenye kupoteza, na kutokana na fitina za mauti, yaani muda wa kukata roho, tusije kupinda tukatoka katika Uislamu au Sunna, au fitina za kaburini kama maswali ya Malaika wawili.
Jambo la nne:Kuomba kinga zitokanazo na fitina za Masihi Dajali atakeyetokea zama za mwisho, Mwenyezi Mungu atawapa mtihani waja wake kupitia yeye; na Mtume kamtaja kwa jina kutokana na ukubwa wa fitina zake.