1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti
  3. Fiq'hi na misingi yake.

Hadithi Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu, kisha akaja katika swala ya Ijumaa akasikiliza na akanyamaza atasamehewa yale yaliyoko kati ya Ijumaa yake hiyo na Ijumaa ijayo na ziada ya siku tatu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَنْ تَوَضَّأَ فَأَحْسَنَ الْوُضُوءَ ثُمَّ أَتَى الْجُمُعَةَ فَاسْتَمَعَ وَأَنْصَتَ غُفِرَ لَهُ مَا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الْجُمُعَةِ وَزِيَادَةُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ، وَمَنْ مَسَّ الْحَصَى فَقَدْ لَغَا».

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu, kisha akaja katika swala ya Ijumaa akasikiliza na akanyamaza atasamehewa yale yaliyoko kati ya Ijumaa yake hiyo na Ijumaa ijayo na ziada ya siku tatu, na atakayegusa kijiwe basi atakuwa kafanya mchezo"

Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim Swahiih Muslim - 857

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kutawadha na akaufanya vyema udhu wake kwa kukamilisha nguzo zake na kufuata Sunna zake na adabu zake, kisha akaswali swala ya Ijumaa na akanyamaza na kumsikiliza mhutubu, na akanyamaza pasina kuleta mazungumzo yasiyofaa; Basi Mwenyezi Mungu atamsamehe madhambi yake madogo kwa muda wa siku kumi, kuanzia sala ya Ijumaa hadi Ijumaa ya pili na ziada ya siku tatu, kwa sababu jambo jema huzidishwa mara kumi. Kisha rehema na amani ziwe juu yake akatahadharisha juu ya moyo kutojali mawaidha yanayosemwa katika hotuba, na kuchezea viungo kwa kugusa kokoto na aina nyinginezo za upuuzi na kujishughulisha, hayo yote ni katika aina ya mchezo na kujishughulisha kusikofaa, kwani mwenye kufanya hivyo atakuwa kafanya mchezo, na atakayefanya mchezo atakuwa hana fungu kamili katika ujira wa swala ya Ijumaa.

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo la kutawadha na kuukamilisha kikamilifu, na kushikamana na sala ya Ijumaa.
  2. Fadhila za swala ya Ijumaa.
  3. Ulazima wa kunyamaza kwa ajili ya hotuba ya Ijumaa, na kutojishughulisha kwa mazungumza au kinginecho.
  4. Iwapo mtu atafanya mchezo wakati wa hotuba Swala ya Ijumaa itakuwa sahihi na haitomlazimu kurudia swala ya faradhi, isipokuwa itakuwa na upungufu wa malipo.

Kuonyesha Tafsiri

53 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
KY Кыргызча القيرقيزية
NE नेपाली النيبالية
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
CS Čeština التشيكية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
AZ Azərbaycan الأذربيجانية
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية