عَنْ سَهْلِ بْنِ مُعَاذِ بْنِ أَنَسٍ عَنْ أَبِيهِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَنْ أَكَلَ طَعَامًا فَقَالَ: الحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَطْعَمَنِي هَذَا وَرَزَقَنِيهِ مِنْ غَيْرِ حَوْلٍ مِنِّي وَلاَ قُوَّةٍ، غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ».
[حسن] - [رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه وأحمد] - [سنن الترمذي: 3458]
المزيــد ...
Kutoka kwa Sahal bin Muadhi bin Anas kutoka kwa baba yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Atakayekula chakula, akasema: Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyenilisha chakula hiki, na akaniruzuku, si kwa ujanja wangu wala kwa nguvu zangu, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia".
[Ni nzuri] - - [سنن الترمذي - 3458]
Anamhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kula chakula amshukuru Mwenyezi Mungu, kuwa mimi sina uwezo wa kuleta chakula wala kukila isipokuwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na msaada wake, Kisha akatoa habari njema rehema na amani ziwe juu yake kwa yeyote atakayesema hivyo kuwa anastahili msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa dhambi zake ndogo ndogo zilizopita.