عن عمران بن حصين رضي الله عنه وابن عباس رضي الله عنهما مرفوعاً: «ليس منا من تَطَيَّر أو تُطُيِّر له، أو تَكَهَّن أو تُكِهِّن له، أو سحَر أو سُحِر له؛ ومن أتى كاهنا فصدَّقه بما يقول؛ فقد كفر بما أنزل على محمد صلى الله عليه وسلم ».
[صحيح] - [رواه البزار عن عمران بن حصين -رضي الله عنهما-. ورواه الطبراني في الأوسط عن ابن عباس -رضي الله عنهما]
المزيــد ...

Kutoka kwa Imran Bin Huswain- Radhi za Allah ziwe juu yake-na Ibni Abbas- Radhi za Allah ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Sio miongoni mwetu mwenye kuitakidi mikosi kupitia ndege, au mwenye kuwa kuhani au akafanyiwa ukuhani, au akafanya uchawi, au akataka afanyiwe uchawi, na atakaye muendea kuhani na akamsadikisha ayasemayo, basi huyo kayakufuru aliyokuja nayo Muhammad- Rehma na amani ziwe juu yake".
Sahihi - Imepokelewa na Albazaar

Ufafanuzi

Amesema Mtume-Rehma na amani ziwe juu yake-" Hawi ni katika wafuasi wetu wenye kufuata sharia zetu mwenye kuitakidi nuksi katika vitu, ukuhani , mwenye kufanya uchawi au akafanyiwa vitu hivi,maana katika kufanya hayo ni kujifanya kujua ghaibu,jambo ambalo ni la Allah pekee, na jambo hilo linaiharibu itikadi ya mtu na akili yake, na atakaye msadikisha mwenye kuyafanya haya atakuwa kaukufuru wahyi wa Allah ambao umekuja kubatilisha mambo haya ya kijahili,na kuikinga akili na mambo haya; Na inajumuishwa vilevile na mambo haya,mambo wanayoyafanya baadhi ya watu ya kusoma viganja vya watu au kwenye vikombe,au kuzifungamanisha nyota mafanikio au kufeli kwa mtu na mfano wa hayo. Na wamebainisha maimamu wawili,Imammu Albaghawi na Ibnu Taymiyya,maana ya neno Arraaf,na Kuhani,na Mnajimu,na anayetazamia kwa kupitia mchanga,wakasema: Kila mwenye kudai kujua chochote katika mambo ya ghaibu basi ima ataitwa kuhani au atakuwa anashirikiana nae katika baadhi ya sifa,maana kuhani ni yule mwenye kueleza mambo ambayo hayajatokea,na taarifa hizo anazipata kwa mashaitwani wanaokwenda kusikiliza habari za mbinguni.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani
Kuonyesha Tarjama

Faida nyingi

  1. Uharamu wa kudai kujua ghaibu; kwasababu inapingana na tauhidi.
  2. Uharamu wa kumsadikisha mwenye kufanya hivyo kwa ukuhani au kinginecho; kwasababu ni kufuru.
  3. Ulazima wa kumpinga kuhani na mfano wake, na ulazima wa kujiweka mbali nao, na elimu zao.
  4. Ulazima wa kushikamana na yale yaliyoteremshwa kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, na kuyaacha yanayokwenda kinyume naye.
  5. Uharamu wa mikosi na uchawi na ukuhani.
  6. Uharamu wa kuomba kufanyiwa mambo haya matatu.
  7. Nikuwa Qur'ani imeteremshwa na wala haikuumbwa.