عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال: لمَّا ثَقُل النبي صلى الله عليه وسلم جَعَل يَتَغَشَّاه الكَرب، فقالت فاطمة رضي الله عنها : واكَربَ أَبَتَاه، فقال: «لَيسَ عَلَى أَبِيك كَرب بعد اليوم». فلما مات، قالت: يا أَبَتَاه، أجاب ربًّا دَعَاه! يا أبَتَاه، جَنَّة الفِردَوس مَأوَاه! يا أبتاه، إلى جبريل نَنعَاه! فلمَّا دُفِن قالت فاطمة رضي الله عنها : أَطَابَت أَنفُسُكُم أَن تَحثُوا عَلَى رسُولِ الله صلى الله عليه وسلم التُّراب؟!
[صحيح] - [رواه البخاري]
المزيــد ...

Kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: alipozidiwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akawa anagubikwa na matatizo (kilevi cha kifo -sakaratil mauti), akasema Fatma: Nalia kwa matatizo ya baba yangu, akasema: "Hakuna kwa baba yako matatizo baada ya leo". Basi alipofariki Fatma -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- alisema: Ewe baba yangu, kamuitikia Mola aliyemuita! Ewe baba yangu, pepo ya Firdausi ndiyo mafikio yake, Ewe baba yangu, kwa Malaika Jibril ndiko tunako tangaza msiba wake, alipozikwa alisema Fatma -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Hivi zimeridhika nafsi zenu kumwaga udongo juu ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-?!
Sahihi - Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Ufafanuzi

Inatupa picha hadithi hii juu ya subira ya Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- juu ya kilevi cha kifo, alipozidiwa katika maradhi ambayo alifariki kwaajili yake, akawa anagubikwa na shida kutokana na ukali wa yale yanayompata; kwasababu yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- yanamzidia maumivu na maradhi, na hii ni kwasababu ya hekima ya hali ya juu: ili ayafikie yale yalioko kwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa daraja za juu kwasababu ya malipo ya subira yake, kila anapofunikwa na shida Fatma -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- anasema: "Nalia kwa misukosuko ya baba yangu" anaumia kwasababu ya matatizo yanaomfika, kwasababu yeye ni mwanamke, na mwanamke huwa hawezi kuvuta subira. Akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Hakuna kwa baba yako matatizo baada ya leo"; kwasababu yeye Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alipohama kutoka duniani kahamia kwa rafiki aliyejuu, kama alivyokuwa -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema wakati akikumbwa na shida za kifo- "Ewe Mola wangu kwa rafiki aliyejuu, Ewe Mola wangu kwa rafiki aliyejuu, huku akitazama katika paa la nyumba -Rehema na Amani ziwe juu yake-". Alipofariki Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akawa -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akimlilia kwa huzuni, lakini ilikuwa chinichini (haikuwa kwa makelele), na wala haimaanishi kuchukizwa na maamuzi ya Mwenyezi Mungu na mipango yake. Na kauli yake: "Kamuitikia Mola aliyemuita"; Ni kwasababu Mwenyezi Mungu ndiye ambaye mkononi mwake kuna ufalme wa kila kitu, na ajali za viumbe ziko mkononi mwake. kamuitikia muitaji wa Mwenyezi Mungu, nayo nikuwa yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- atakapokufa atakuwa kama wengineo katika waumini, inapandishwa roho yake mpaka isimamishwe mbele ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka juu ya mbingu ya saba. Na kauli yake: "Ewe baba yangu pepo ya Firdausi ndiyo mafikio yake" -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwasababu yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- ndio kiumbe mwenye nafasi ya juu kuliko wote peponi, kama alivyosema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Niombeeni mimi utetezi; kwani hiyo ni nafasi peponi ambayo haistahiki kwa yeyote ila kwa mja miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu, na ninataraji mimi kuwa ndiye mwenye nafasi hiyo", na wala haina shaka kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- mafikio yake ni pepo ya Firdausi, na pepo ya Firdausi ndiyo daraja ya juu zaidi katika daraja za pepo, na paa lake lililo juu yake ni Arshi ya Mola Aliyetakasika na kutukuka, na Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- yuko daraja ya juu zaidi kuliko hiyo. Kauli yake: "Ewe baba yangu kwa Jibrili ndiko tunako tangaza msiba wake" Na akasema: Hakika sisi tunatoa habari za kifo chake kwa Jibrili kwasababu Jibrili ndiye aliyekuwa akimuijia akimfundisha kwa wahyi zama za uhai wake, na wahyi umefungamana na uhai wa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-. Kisha pindi alipobebwa na akazikwa, alisema -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Hivi nafsi zenu zimeridhika kumwaga udongo juu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-? Yaani hii ni kwasababu ya huzuni yake kubwa juu yake, na huzuni yake na maumivu yake ni kwa kutengana na mzazi wake, na kujua kwake kuwa maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Mwenyezi Mungu alizijaza nyoyo zao mapenzi ya Mtume -Ziwe juu yake Rehema na Amani- aliwauliza swali hili, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu yeye ndiye mwenye maamuzi, na marejeo ni kwake, na kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kitabu chake: (Hakika wewe ni maiti na hakika wao ni maiti).

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Kikurdi Kireno
Kuonyesha Tarjama