+ -

عَنْ أَبِي أَيُّوبَ الأَنْصَارِيِّ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِذَا أَتَيْتُمُ الغَائِطَ فَلاَ تَسْتَقْبِلُوا القِبْلَةَ، وَلاَ تَسْتَدْبِرُوهَا وَلَكِنْ شَرِّقُوا أَوْ غَرِّبُوا» قَالَ أَبُو أَيُّوبَ: فَقَدِمْنَا الشَّأْمَ فَوَجَدْنَا مَرَاحِيضَ بُنِيَتْ قِبَلَ القِبْلَةِ فَنَنْحَرِفُ، وَنَسْتَغْفِرُ اللَّهَ تَعَالَى.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 394]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ayub Al-Answari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
“Mnapoingia chooni, msielekee Kibla, wala msikipe mgongo, bali elekeeni Mashariki au Magharibi.” Abuu Ayub akasema: Basi tukaenda Sham tukakuta vyoo vimejengwa kuelekea Kibla, tukawa tunageuka, na tunaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 394]

Ufafanuzi

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mwenye kutaka kukidhi haja kubwa au ndogo kuelekea Kibla na upande wa Al-Kaaba, na asiigeuze kwa kuiweka nyuma ya mgongo wake. Bali ni lazima ageuke akiwa ndani kuelekea Mashariki au Magharibi ikiwa Kibla chake ni kama kibla cha watu wa Madina. Kisha Abuu Ayub (radhi za Allah ziwe juu yake) akaeleza kuwa walipofika Sham walikuta vyoo vilivyotayarishwa kwa ajili ya kujisaidia vimejengwa kuelekea Al-Kaaba, hivyo wakawa wakijigeuza kutoka upande wa Kibla, pamoja na hivyo bado wanamuomba msamaha Mwenyezi Mungu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Hekima ya kufanya hilo ni kuitukuza Al-Kaaba tukufu na kuiheshimu.
  2. Kuomba msamaha kwa Allah baada ya kutoka mahali pa kukidhi haja.
  3. Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake; Kwa sababu alipoeleza lililokatazwa akaelekeza linalofaa.