+ -

عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعًا: «اسْتَنْزِهوا من البول؛ فإنَّ عامَّة عذاب القبر منه».
[صحيح] - [رواه الدارقطني]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, Hadithi Marfu'u: "Jisafisheni vizuri kutokana na mkojo; kwani adhabu nyingi za kaburini zinatokana na hilo".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Addaar- Alqutni]

Ufafanuzi

Anatubainishia Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake katika hadithi hii kuwa moja ya sababu za adhabu za kaburi, ni hii iliyoenea sana, nayo nikutojisafisha vizuri na kujitwaharisha kutokana na mkojo.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Kijapani Pashto Kiassam Albanian
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuchunga juu ya kujisafisha na kujiweka mbali na mkojo, ili usimpate katika mwili wake wala nguo yake.
  2. Lililo bora ni kufanya haraka kuosha mahala hapo, na kujitwaharisha baada ya kupatwa; ili asiambatane na najisi, ama uwajibu wa kuiondoa unakuwa wakati wa swala.
  3. Nikuwa mkojo ni najisi, ukiupata mwili au nguo au sehemu, unapanajisisha; Hivyo haiswihi swala kwa hilo; kwasababu kujisafisha kutokana na najisi ni moja kati ya sharti zake.
  4. Nikuwa kuacha kujisafisha kutokana na mkojo ni katika madhambi makubwa.
  5. kuthibiti kwa adhabu za kaburini, nazo zimethibiti kwa Qur'ani na sunna na makubaliano ya wanachuoni.
  6. Kuthibitisha malipo Akhera, Hivyo sehemu ya kwanza katika vituo vya akhera ni kaburi: Ima iwe ni kiwanja miongoni mwa viwanja vya pepo, au shimo katika mashimo ya moto.