+ -

عَنْ عَمْرِو بْنُ سُلَيْمٍ الأَنْصَارِيُّ قَالَ: أَشْهَدُ عَلَى أَبِي سَعِيدٍ قَالَ: أَشْهَدُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«الغُسْلُ يَوْمَ الجُمُعَةِ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُحْتَلِمٍ، وَأَنْ يَسْتَنَّ، وَأَنْ يَمَسَّ طِيبًا إِنْ وَجَدَ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 880]
المزيــد ...

Kutoka kwa Amri Bin Suleim Al-Answari amesema: Ninamshuhudilia Abuu Saidi kuwa alisema: Ninamshuhudilia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwa alisema:
"Kuoga siku ya Ijumaa ni wajibu kwa kila aliyebaleghe, na apige mswaki, na aguse marashi ikiwa atapata".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 880]

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kuoga siku ya Ijumaa kumetiliwa mkazo ni sawa na wajibu upande wa kila aliyebalehe katika waislamu waliowajibikiwa na Ijumaa, Na asafishe meno yake kwa mswaki na mfano wake, na ajitie manukato kwa harufu yoyote nzuri ya uturi.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumetiwa mkazo kuoga siku ya Ijumaa kwa kila mwanaume wa kiislamu aliyebaleghe.
  2. Usafi na kuondoa harufu mbaya ni jambo linalotakiwa na ni sheria kwa muislamu.
  3. Kuitukuza siku ya Ijumaa, na kujiandaa kwa ajili yake.
  4. Mkazo wa kutumia mswaki siku ya Ijumaa.
  5. Sunna ya kujipaka manukato kwa harufu yoyote nzuri kabla ya kwenda katika swala ya Ijumaa.
  6. Mwanamke akitoka nyumbani kwake kwa ajili swala ua kinginecho, haifai kwake kujitia manukato; kwa sababu mafundisho ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yamekataza hilo.
  7. Anayejiotea ni mtu aliyebaleghe, na kubaleghe hutokea kwa alama mbali mbali, tatu kati yake wanashirikiana wanaume na wanawake nazo ni: Ya kwanza: Kukamilisha miaka kumi na tano. Ya pili: Zikiota nywele pembezoni mwa tupu. Ya tatu: Kushusha manii kwa kujiotea au kwa matamanio au bila matamanio. Ama alama ya nne: Hii inamuhusu mwanamke, nayo ni: Hedhi, mwanamke akipata hedhi, anakuwa tayari kabaleghe.