عن أنس بن مالك -رضي الله عنه- أن النبي صلى الله عليه وسلم كان إذا دخل الخَلاء قال: ((اللهم إني أَعُوذ بك من الخُبُثِ والخَبَائِث)).
[صحيح.] - [متفق عليه.]
المزيــد ...

Kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake alikuwa pindi anapoingia chooni anasema: (Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na mashetani wa kiume na mashetani wa kike)
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Anatuelezea Anasi bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- naye ndiye aliyepata heshima ya kumuhudumia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi hii adabu za kiutume wakati wa kukidhi haja, nayo nikuwa yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- kutokana na kupenda kwake zaidi na kuelekea kwake zaidi kwa Mola wake alikuwa haachi kumtaja na kutaka msaada kwake katika hali yoyote, basi yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa anapotaka kuingia mahala ambapo atakidhi haja yake anataka msaada kwa Mwenyezi Mungu, na akijiegemeza kwake ili amkinge na mashetani ya kiume na ya kike; kwasababu wao ndio wanaojaribu kwa kila namna kuhakikisha wanamuharibia muislamu jambo la dini yake na ibada yake, na umefasiriwa uchafu kidogo (Khubuthi) na uchafu mwingi (khabaaithi) kuwa ni shari na najisi. Na sababu ya kuomba kinga nikuwa nyumba ya kukidhi haja, yaani choo, ni sehemu za mashetani, na alisema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Hakika maeneo ya udhu hufikiwa (yaani na mashetani), atakapoingia mmoja wenu basi na aseme: Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na mashetani wa kiume na mashetani wa kike" kaipokea bin Maajah na wengineo na akaisahihisha Al Albaaniy, na pia kuna sababu nyingine nayo nikuwa mwanadamu anahitaji kufunua uchi wake pindi atakapoingia sehemu hizi, Na alisema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Sitara iliyoko baina ya majini na uchi wa mwanadamu pindi anapoingia chooni ni aseme: Bismillaah -kwa jina la Mwenyezi Mungu" kaipokea bin Maajah na wengineo na akaisahihisha Al Albaaniy pia.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama