عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ:
إِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى أَنْ يُسْتَنْجَى بِرَوْثٍ أَوْ عَظْمٍ، وَقَالَ: «إِنَّهُمَا لَا تُطَهِّرَانِ».
[صحيح] - [رواه الدارقطني] - [سنن الدارقطني: 152]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekataza kustanji kwa kinyesi cha wanyama au mfupa, na akasema: "Vitu hivyo havisafishi sawa sawa".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Addaar- Alqutni] - [سنن الدارقطني - 152]
Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekidhi haja yake sawa iwe haja ndogo au kubwa, kustanji kwa mfupa wa mnyama au kinyesi chake na mabaki yake yaliyokauka; na akasema: Hivyo haviondoshi najisi, na wala havisafishi vizuri.