عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه قال: كان رسول الله صلى الله عليه وسلم أَشَدَّ حياءً من العَذْرَاءِ في خِدْرِهَا، فإذا رأى شيئا يَكْرَهُهُ عرفناه في وجهه.
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Saidi Al khudriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Alikuwa Mtume Rehema na Amani zimfikie na haya (aibu) nyingi kuliko msichana bikra akiwa chumbani kwake, alikuwa akiona kitu asichokipenda basi tunajua kwa kumtazama usoni kwake.
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na aibu sana kuliko mwanamke ambaye hajawahi kuolewa, naye ndiye mwanamke mwenye haya kubwa kuliko wanawake wote; kwasababu hajawahi kuolewa na hajawahi kuishi na wanaume, utamuona akiwa na haya chumbani kwake, hivyo Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ana haya kubwa zaidi kuliko yake, lakini yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapoona anachokichukia na yale yanayokwenda kinyume na tabia yake -Rehema na Amani ziwe juu yake- lilikuwa likijulikana hilo usoni mwake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kireno
Kuonyesha Tarjama