عن زينب بنت جحش رضي الله عنها أنَّ النبي صلى الله عليه وسلم دخل عليها فَزِعًا، يقول: «لا إله إلا الله، وَيْلٌ لِلْعَرَبِ مِنْ شَرٍّ قد اقْتَرَب، فُتِحَ اليوم من رَدْمِ يَأْجُوجَ ومَأجُوجَ مثل هذه»، وحلَّق بأُصبُعيه الإبهامِ والتي تَلِيها، فقلت: يا رسول الله، أنَهْلِكُ وفينا الصَّالِحُون؟ قال: «نعم، إِذَا كَثُرَ الخَبَثُ».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Zainab bint Jahshi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- aliingia kwake akiwa na hali ya mfadhaiko, akisema: "Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, Ole wao waarabu kutokana na shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya-ajuju na Ma-juju mfano wa hiki, na akachora duara kwa vidole vyake viwili, kidole gumba na kile kinachofuata, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Hivi tunaweza kuangamizwa hali miongoni mwetu kuna wema? Akasema: Ndiyo, pindi uchafu utakapokithiri".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Kutoka kwa mama wa waumini Zainab binti Jahshi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- aliingia kwake hali uso wake ukiwa mwekundu, akisema: "Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu" akiithibitisha tauhidi na akiituliza nafsi. kisha akawatahadharisha waarabu akasema: Ole wao waarabu, kutokana na shari iliyokaribia", kisha akabainisha kuwa shari hii nikuwa imefunguliwa nafasi ndogo katika ngome ya Ya-ajuju na Ma-ajuju, kwa kiasi cha mduara uliyoko baina ya vidole viwili kidole cha shahada na kidole gumba. Akasema Zainab: "Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Je, hivi tunaweza kuangamia hali yakuwa miongoni mwetu kuna watu wema?, Akaeleza kuwa mwema haangamii, bali yeye ni mwenye kusalimika mwenye kuokoka; lakini machafu yakikithiri na mwema pia anaangamia, yatakapokithiri matendo machafu mabaya katika jamii hata kama watakuwa ni waislamu na yakawa hayakukemewa, basi wao watakuwa wamezitia nafsi zao katika maangamivu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama