عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما أن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«الرَّاحِمُونَ يَرْحَمُهمُ الرَّحمنُ، ارحَمُوا أهلَ الأرضِ يَرْحْمْكُم مَن في السّماء».
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي وأحمد] - [سنن أبي داود: 4941]
المزيــد ...
Imepokewa Kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Wenye huruma huwahurumia Ar-Rahmani -Mwingi wa huruma-, wahurumieni walioko ardhini atakuhurumieni aliyeko mbinguni."
[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 4941]
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa wale wenye kuwahurumia wenzao huwahurumia Rahman -Mwingi wa rehema- kwa huruma yake iliyokienea kila kitu; Yakiwa ni malipo sawa na matendo yao.
Kisha akaamrisha -Rehema na amani ziwe juu yake-kuwahurumia wote walioko ardhini kwanzia binadamu au wanyama au ndege, au wengineo katika aina ya viumbe mbali mbali, na malipo ya hilo; mtahurumiwa na Mwenyezi Mungu kutoka juu ya mbingu yake ya saba.