+ -

عن أُبيِّ بن كعبٍ رضي الله عنه قال:
صلَّى بنا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يومًا الصُّبحَ فقال: «أشاهِد فُلان؟» قالوا: لا، قال: «أشاهِدٌ فُلان؟» قالوا: لا، قال: «إنَّ هاتيَنِ الصَّلاتين أثقَلُ الصَّلَواتِ على المُنافقين، ولو تعلمون ما فيهما لأتيتُمُوهما ولو حَبْوًا على الرُّكب، وإن الصفَّ الأوّلَ على مِثلِ صَفِّ الملائكة، ولو عَلِمتُم ما فضيلتُه لابتَدَرتُموهُ، وإنّ صلاةَ الرجل مع الرجل أزكى من صلاتِه وحدَه، وصلاتَه مع الرجلَين أزكى من صلاتِه مع الرجل، وما كَثُرَ فهو أحبُّ إلى الله تعالى».

[صحيح] - [رواه أبو داود والنسائي وأحمد] - [سنن أبي داود: 554]
المزيــد ...

Kutoka kwa Ubai bin Ka'ab radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Alitusalisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala ya asubuhi, akasema: "Hivi fulani yupo", Wakasema: Hapana, akasema: "Na je fulani yupo?", Wakasema: Hapana: Akasema: "Hakika swala hizi mbili, ni swala nzito sana kwa wanafiki, na lau kama mngejua malipo yaliyomo basi mngezijia, hata kwa kutambaa kwa magoti, na hakika safu ya kwanza iko katika mithili ya safu ya Malaika, na laiti mngejua ni zipi fadhila zake basi mngezijia haraka mno, na hakika swala ya mtu na mwenzie ni safi zaidi kuliko swala yake peke yake, na swala yake akiwa na watu wawili ni nzuri zaidi kuliko swala yake na mtu mmoja, na wingi unavyozidi ndio unaopendeka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu".

[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 554]

Ufafanuzi

Siku moja alisali Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala ya Alfajiri, kisha akauliza: Je, fulani kahudhuria nasi swala yetu hii? Maswahaba wakasema: Hapana. Kisha akasema: Hivi fulani kahudhuria? kwa mtu mwingine, wakasema: Hapana. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika swala ya Alfajiri na Ishaa ni swala nzito kwa wanafiki; kwa sababu ya kuzidi kwa uvivu katika nyakati hizi, na ni kwa sababu ya uchache wa kutoonekana kwa watu, kwa sababu gizani hawaonekani.
Na lau kama mngejua enyi waumini yaliyomo ndani ya swala hizi mbili Alfajiri na Ishaa katika malipo na thawabu za ziada, kwa sababu malipo huwa kwa kadiri ya tabu, basi mgeziendea hata kwa kutambaa na kwa kutembea kwa mikono na magoti.
Na hakika safu ya kwanza katika ukaribu wake na imam ni kama safu za Malaika ukaribu wake na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na lau waumini wangelijua ni zipi fadhila za safu ya kwanza basi wangeshindana kuiwahi, Hakika swala ya mtu na mtu mwingine inamalipo makubwa na ina athari kubwa kuliko swala yake peke yake, na swala yake pamoja na watu wawili ni bora kuliko swala yake na mtu mmoja, Na swala ambayo waswaliji watakuwa wengi hiyo ndio swala bora inayopendeka kwa Mwenyezi Mungu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda malgaashka
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Sheria ya imam wa msikiti kukagua hali za waumini, na kumuulizia asiyekuwepo.
  2. Kudumu na swala ya jamaa, na hasa hasa swala ya Ishaa na Alfajiri ni katika alama za imani.
  3. Ukubwa wa malipo ya swala mbili, Ishaa na Alfajiri; kwa sababu kuziendea kunahitaji kupambana na nafsi na kuwa na subira katika utiifu, ikawa malipo yake ni makubwa kuliko swala zingine.
  4. Swala ya jamaa inakamilika kwa kuanzia watu wawili na zaidi.
  5. Kumebainishwa fadhila za safu ya kwanza, na himizo la kuiendea haraka.
  6. Fadhila za wingi wa jamaa, kwani kila wingi unavyokithiri pia malipo huwa mengi.
  7. Amali njema hutofautiana ubora kulingana na kuzidiana sheria yake, na hali zake maalum.