عن أبي هريرة، قال: أتَى النبي صلى الله عليه وسلم رجُلٌ أعْمَى، فقال: يا رسول الله، إنه ليس لي قائد يَقُودُني إلى المسجد، فَسَأل رسول الله صلى الله عليه وسلم أن يُرَخِّص له فيصلِّي في بَيْتِه، فرَخَّص له، فلمَّا ولىَّ دَعَاه، فقال: «هل تسمع النِّداء بالصلاة؟» قال: نعم، قال: «فأجِب».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira, Amesema: Alimuijia Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake mtu kipofu, Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika sina muongozaji wa kuniongoza njia kuja msikitini, akamuomba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake amruhusu aswalie nyumbani kwake, akamruhusu, alipogeuka kuondoka akamuita, kisha akasema: "Je unasikia wito wa swala?" Akasema: Ndiyo, akasema: "basi itikia wito wa sala".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Alikuja mtu kipofu kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mtu kipofu sina wa kunisaidia na kunishika mkono mpaka msikitini, katika swala tano, akitaka amruhusu Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- kuacha jamaa, akamruhusu, alipogeuka kuondoka akamuita na akasema: Je unasikia adhana ya swala? Akasema: Ndiyo. Akasema: Basi muitike mnadi swala.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Uwajibu wa swala ya jamaa; kwasababu ruhusa haiwi ispokuwa kwa kitu ambacho ni cha lazima na wajibu, kisha kauli yake: "Muitike" Hii ni amri, na kimsingi nikuwa amri huwa ni ya kuwajibisha.
  2. Uwajibu wa swala ya jamaa kwa kipofu hata kama atakuwa hana muongozaji wa kumuongoza kwenda msikitini.
  3. Kumlea mtoa majibu(Fat-wa) katika kuacha kufanya haraka katika kutoa majibu nakuwa anatakiwa atake ufafanuzi wa hali ya muulizaji kabla ya kutoa majibu.