عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللهِ رضي الله عنهما أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«إِذَا دَخَلَ الرَّجُلُ بَيْتَهُ، فَذَكَرَ اللهَ عِنْدَ دُخُولِهِ وَعِنْدَ طَعَامِهِ، قَالَ الشَّيْطَانُ: لَا مَبِيتَ لَكُمْ، وَلَا عَشَاءَ، وَإِذَا دَخَلَ، فَلَمْ يَذْكُرِ اللهَ عِنْدَ دُخُولِهِ، قَالَ الشَّيْطَانُ: أَدْرَكْتُمُ الْمَبِيتَ، وَإِذَا لَمْ يَذْكُرِ اللهَ عِنْدَ طَعَامِهِ، قَالَ: أَدْرَكْتُمُ الْمَبِيتَ وَالْعَشَاءَ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2018]
المزيــد ...
ImepokelewaKutoka kwa Jabir radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, hakika yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Anapoingia mtu nyumbani kwake akamtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia kwake na wakati wa chakula chake, Shetani husema: Hakuna malazi kwenu, wala chakula cha usiku, na anapoingia na hakumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia kwake, Shetani husema: Mmepata malazi, na asipomtaja Mwenyezi Mungu wakati wa chakula chake, husema: Mmepata malazi na chakula cha usiku".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2018]
Ameamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumtaja Allah wakati wa kuingia nyumbani na kabla ya kupata chakula, nakuwa mtu akimtaja Mwenyezi Mungu kwa kusema: (Bismillaah) -Naanza kwa jina la Mwenyezi Mungu- wakati wa kuingia nyumbani kwake na wakati wa chakula chake, Shetani husema kuwaambia wasaidizi wake: Hamna bahati leo ya kupata malazi wala chakula cha usiku ndani ya nyumba hii ambayo mwenye nyumba kajilinda kutokana nanyi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ama mtu akiingia nyumbani kwake na akawa hakumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia kwake wala wakati wa kupata kwake chakula, Shetani huwaeleza wasaidizi wake kuwa wamepata mahali pa kulala, na chakula cha usiku ndani ya nyumba hii.