عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ:
تَوَضَّأَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَرَّةً مَرَّةً.
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 157]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema:
Alitawadha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mara moja moja.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 157]
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya nyakati zake anapotawadha anaosha kila kiungo katika viungo vya udhu mara moja moja, anaosha uso pamoja kusukutua na kupandisha maji puani, na mikono miwili na miguu miwili mara moja moja, na hiki ndicho kiwango cha wajibu.