عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ زَيْدٍ رضي الله عنه:
أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ تَوَضَّأَ مَرَّتَيْنِ مَرَّتَيْنِ.
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 158]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdallah bin Zubairi -Radhi za Allah ziwe juu yake-:
Anasimulia kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitawadha mara mbili mbili.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 158]
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya nyakati zake anapotawadha anaosha kila kiungo katika viungo vya udhu mara mbili, anaosha uso ikiwemo kusukutua na kupandisha maji puani na mikono miwili na miguu miwili mara mbili.