عن عمران بن حصين رضي الله عنهما قال: كانت بي بَوَاسيرُ، فسألت النبي صلى الله عليه وسلم عن الصلاة، فقال: «صَلِّ قائما، فإن لم تستطع فقاعدا، فإن لم تستطع فعلى جَنْبٍ».
[صحيح] - [رواه البخاري]
المزيــد ...

Kutoka kwa Imran bin Huswain- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: Nilipatwa na bawasiri (ugonjwa unaosababisha uvimbe sehemu ya siri ya nyuma) Nikamuuliza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- kuhusu swala, Akasema: "Swali ukiwa umekaa, ikiwa hutoweza basi ukiwa umekaa, ikiwa hutoweza basi ukiwa umelalia ubavu".
Sahihi - Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Ufafanuzi

Inabainisha hadithi tukufu namna ya kuswali kwa atakayekuwa na maradhi ya bawasiri au maumivu wakati wa kusimama na mfano wa hayo katika nyudhuru, Akaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa asili ni kusimama, ispokuwa katika hali ya kutoweza, basi aswali akiwa amekaa, na ikiwa hatoweza kuswali akiwa kakaa basi anaweza kuswali kwa ubavu wake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Ulazima wa kuchunga daraja za swala ya mgonjwa katika swala za faradhi, ni wajibu kwake kusimama akiweza, kwasababu hiyo ni nguzo katika nguzo za swala ya faradhi, hata kama ni kwa kuegemea, au kujishikiza katika kitu kama fimbo, au ukuta, au mfano wa hicho.
  2. Atakayeshindwa kusimama, au kukawa ni tabu kwake, basi atalazimika kukaa, walau hata kwa kujiegesha au kuegemea, na atarukuu na atasujudu akiwa na uwezo juu ya hilo, ikiwa hatoweza kukaa, au ikawa ni tabu kwake basi ataswali kwa ubavu wake, na ubavu wa kulia ndio bora, ikiwa ataswali chali (kwa kulalia mgongo) upande wa kibla itafaa, ikiwa hatoweza basi ataashiria tu kwa kichwa chake, na kunakuwa kuashiria kwake kwa kusujudu kumeinama zaidi kuliko kuashiria kwake kwa kurukuu, kwaajili ya kutofautisha kati ya nguzo mbili, na kwakuwa sijida huwa imeinama zaidi kuliko rukuu.
  3. Asihame kutoka hali moja kwenda nyingine kwa kufanya kidogo kuliko ya mwanzo ispokuwa wakati wa kushindwa, au wakati wa kupata tabu katika hali ya kwanza, au katika kuitekeleza; kwasababu kuhama kutoka hali moja kwenda nyingine kumewekewa sharti la kushindwa.
  4. Kiwango cha tabu ambacho ni halali kuswali swala ya faradhi kwa kukaa, ni tabu ambazo zitamkosesha unyenyekevu; hiyo ni kwasababu utulivu ndio kusudio kubwa la swala.
  5. Nyudhuru ambazo zina halalisha swala ya faradhi kwa kukaa ni nyingi, si maalumu kwa maradhi pekee, kama ufupi wa paa la nyumba ambayo hawezi kutoka ndani yake, na kuswali katika boti, au meli, au gari, au ndege kunapokuwa na haja ya kufanya hivyo, na kushindwa kusimama, zote hizo ni nyudhuru zinazohalalisha hilo.
  6. Swala haidondoki uwajibu wake madamu akili bado iko, mgonjwa asipoweza kuashiria kwa kichwa chake anaashiria kwa macho yake, hivyo atainamisha kidogo kwaajili ya rukuu, na atainamisha sana kwaajili ya sijida, akiweza kusoma kwa ulimi wake atasoma, na asipoweza kuashiria kwa macho yake, ataswali kwa moyo wake.
  7. Lengo la ujumla la hadithi nikuwa yeye ataswali kwa kukaa, kwa mkao wowote atakaotaka, nalo ni makubaliano ya wanachuoni wote, na tofauti ni katika ubora, kwa jopo la wanachuoni wanasema kuwa yeye ataswali kwa kukunja miguu katika sehemu ya kusimama, na baada ya kunyanyuka kutoka katika rukuu, na ataswali kwa mkao wa tahiyatu ndogo katika sehemu ya kunyanyuka kutoka katika sijida.
  8. Nikuwa amri za Mwenyezi Mungu Mtukufu zinaletwa kwa kadiri ya uwezo,hailazimishi Mwenyezi Mungu nafsi ila kwa kadiri ya uwezo wake.
  9. Upole na wepesi wa sheria hii ya kiislamu, nakuwa yenyewe ni kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na hakuweka juu yenu nyinyi uzito katika dini" [Suratul Haji: 78], "Anataka Mwenyezi Mungu akuhafifishieni" [An Nisaa], Hivyo rehma za Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni pana.
  10. Yaliyotangulia ni hukumu ya swala ya faradhi, ama ya sunna inasihi kwa kukaa, hata kama hakuna udhuru, lakini ikiwa kwa udhuru basi malipo yanakuwa yametimia kama kawaida, na bila udhuru ni kwa nusu ya malipo ya swala ya aliyesimama kama ilivyothibiti katika mafundisho Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake.
Ziada