+ -

عَن أَبي عَبْدِ اللهِ الْجَدَلِيِّ قَالَ: سَأَلْتُ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمنينَ رَضيَ اللهُ عنها عَنْ خُلُقِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَتْ:
لَمْ يَكُنْ فَاحِشًا وَلَا مُتَفَحِّشًا وَلَا صَخَّابًا فِي الْأَسْوَاقِ، وَلَا يَجْزِي بِالسَّيِّئَةِ السَّيِّئَةَ وَلَكِنْ يَعْفُو وَيَصْفَحُ.

[صحيح] - [رواه الترمذي وأحمد] - [سنن الترمذي: 2016]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Abdillah Al-Jadali amesema: Nilimuuliza Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake kuhusu tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema:
Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na maneno machafu wala mwenye kujilazimisha machafu, wala hakuwa na makelele masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya, lakini alikuwa akisamehe na kufuta kosa.

[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 2016]

Ufafanuzi

Aliulizwa mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuhusu tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Haikuwa katika tabia zake uchafu na ubaya wa kauli na vitendo, na wala hakuwa akijilazimisha machafu wala kuyakusudia, wala hakuwa mpiga kelele kwa kunyanyua sauti yake masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya; lakini alikuwa akilipa ubaya kwa wema, na akisamehe ndani ya moyo, na akifuta kosa na kulipuuza katika dhahiri.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya kifaransa Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kikurdi Kihausa Kiassam الأمهرية الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa tabia alizokuwa nazo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, tabia za juu na kuwa kwake mbali na tabia mbaya.
  2. Himizo la kufanya tabia njema na kujiweka mbali na tabia mbaya.
  3. Kumekemewa kujilazimisha machafu katika kauli na maneno machafu.
  4. Kumekemewa kunyanyua sauti juu ya watu na kuwapigia makelele.
  5. Himizo la kuukabili ubaya kwa wema, na kusamehe na kufuta kosa.