+ -

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لاَ تَسُبُّوا أَصْحَابِي، فَلَوْ أَنَّ أَحَدَكُمْ أَنْفَقَ مِثْلَ أُحُدٍ ذَهَبًا مَا بَلَغَ مُدَّ أَحَدِهِمْ، وَلاَ نَصِيفَهُ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 3673]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Msiwatukane Maswahaba wangu, kwa sababu, lau kama yeyote kati yenu atatoa dhahabu sawa na (mlima) Uhud (katika njia ya Mwenyezi Mungu), basi haiwezi kuwa sawa na theluthi mbili ya kilo ya mmoja wao wala nusu yake."

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

Ufafanuzi

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwatukana Maswahabah hasa wa mwanzo katika Muhajirina na Ansari; na akaeleza kuwa lau mmoja miongoni mwa watu angetoa dhahabu nyingi kama mlima Uhudi, zisingefikia thawabu zake kwa hilo malipo ya kibaba cha Swahaba mmoja au nusu yake - na kibaba ni kujaza viganja viwili vya mtu wa wastani-; Na hii ni kwa sababu ya ikhilas yao kuwa zaidi, na ukweli wa nia zao, na kuwahi kwao kutoa na kupigana kwao katika njia ya Mwenyezi Mungu kabla ya ufunguzi wa mji wa Makka, ambapo uhitaji wake ulikuwa mkubwa.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya kifaransa Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuwatukana Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao ni haramu, na ni katika maasi makubwa.