عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه:
أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَقُولُ فِي سُجُودِهِ: «اللهُمَّ اغْفِرْ لِي ذَنْبِي كُلَّهُ دِقَّهُ، وَجِلَّهُ، وَأَوَّلَهُ وَآخِرَهُ وَعَلَانِيَتَهُ وَسِرَّهُ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 483]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-:
Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema katika sijida yake: "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe mimi dhambi zangu ndogo zake na kubwa zake za mwanzo wake na mwisho wake, za wazi zake na za siri zake".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 483]
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiomba katika sijida yake akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe madhambi yangu" Kwa kuyasitiri, na unikinge na madhara yake; uyasamehe na usiyatazame na uyafute, "yote", nakusudia: "Za ndani" ndogo zake, na chache zake, "pana zake" kubwa zake na nyingi zake, "za mwanzo wake" dhambi ya kwanza, "na za mwisho zake", na zilizo kati yake, "za wazi zake na siri zake" miongoni mwa zile asizozijua yeyote ila wewe Uliyetakasika.