+ -

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمنين رَضيَ اللهُ عنها قَالَتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«يُحْشَرُ النَّاسُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ حُفَاةً عُرَاةً غُرْلًا» قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ النِّسَاءُ وَالرِّجَالُ جَمِيعًا يَنْظُرُ بَعْضُهُمْ إِلَى بَعْضٍ؟ قَالَ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يَا عَائِشَةُ، الْأَمْرُ أَشَدُّ مِنْ أَنْ يَنْظُرَ بَعْضُهُمْ إِلَى بَعْضٍ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2859]
المزيــد ...

Kutoka kwa Aisha radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Watafufuliwa watu siku ya Kiyama wakiwa peku, uchi, hawajatahiriwa" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wanawake na wanaume wote pamoja, kila mmoja anamtazama mwenzake? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Aisha, jambo litakuwa kubwa mno, kuliko hata mtu kushughulika kumtazama mwenzake".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2859]

Ufafanuzi

Amesimulia Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya yale yatakayokuwa siku ya Kiyama, na kwamba watakusanywa watu baada ya kufufuliwa kutoka makaburini mwao kwa ajili ya hesabu, na hali yao ni kwamba watakuwa miguu peku bila viatu, miili yao ikiwa uchi bila nguo wala kizuizi, na wakiwa hawajatahiriwa kama siku waliyozaliwa na mama zao, aliposikia mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake akasema kwa kustaajabu: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wanawake na wanaume wote pamoja kila mmoja akimtazama mwenzake?! Mtume rehema na amani ziwe juu yake akambainishia: Kwa jambo la kisimamo na kukusanywa baada ya kufufuliwa kutoka katika kifo lina misukosuko kiasi kwamba watu macho yao hayatojali kutazama utupu.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa vitisho vya siku ya Kiyama, na kwamba mtu hakuna kitakachomshughulisha zaidi ya kuwaza hesabu yake na matendo yake.
  2. Msisitizo wa kuwa mwanadamu hatumbukii katika maasi isipokuwa katika hali ya kughafilika; kwani lau akikumbuka ukubwa wa anayemuasi au adhabu zake basi asingeghafilika kumkumbuka na kumshukuru na kufanya vizuri ibada zake hata sekunde moja, na ndio maana utawaona watu siku ya Kiyama wameshughulishwa na nafsi zao, hawatazamani.
  3. Haya kubwa ya wanawake waliokuwa katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kwa mfano huyu hapa Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, anauliza kwa sababu ya aibu, pale anaposikia kwamba viumbe watakusanywa wakiwa uchi wanaume na wanawake.
  4. Amesema Assanadi: Kila mmoja atashughulishwa na jambo lake na wala hatojua hali ya mwenzake, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha" [Abasa: 37] Hakuna yeyote atakayegeuka kutazama uchi wa mwenzake.
  5. Kutahiriwa: Kwa wanaume: Ni kukata ngozi inayositiri kichwa cha uume, na kwa wanawake: Ni kukata kingozi kilichoko juu mahali pa tundu, kinachofanana na kinyama cha jogoo.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama