+ -

عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعاً: يُستجاب لأحدكم ما لم يَعْجَلْ: يقول: قد دعوت ربي، فلم يستجب لي». وفي رواية لمسلم: «لا يزال يُستجاب للعبد ما لم يَدْعُ بإثم، أو قطيعة رحم، ما لم يَسْتَعْجِلْ» قيل: يا رسول الله ما الاستعجال؟ قال: «يقول: قد دعوت، وقد دعوت، فلم أر يستجب لي، فَيَسْتَحْسِرُ عند ذلك ويَدَعُ الدعاء».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- hadithi Marfu'u: "Hujibiwa mmoja wenu anapokuwa hajafanya haraka: anasema: Nimemuomba Mola wangu, na wala sijaona ananijibu mimi" Na katika riwaya ya Muslim: "Hatoacha kuendelea kujibiwa mja madam tu hajaomba dhambi, au kukata ukoo na madam hajafanya haraka" pakasemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kufanya haraka? akasema: "Anasema: Nimeomba, hakika nimeomba, wala sijaona ananijibu, akakata tamaa na wakati huo akaacha kuomba".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwamba hujibiwa mja dua zake madam tu hajaomba kutenda maasi au kukata ukoo, na madam hajafanya haraka, pakasemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kufanya haraka kunakoambatana na kuzuiliwa kujibiwa dua?, akasema: ni mtu kusema: Hakika nimeomba, na nimeomba, na nimerudia rudia kuomba, lakini hajanijibu; akafanya haraka wakati huo na akaacha kuomba.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kireno Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri
Kuonyesha Tarjama