عن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما مرفوعاً: «لا تدعوا على أنفسكم؛ ولا تدعوا على أولادكم، ولا تدعوا على أموالكم، لا توافقوا من الله ساعة يُسأل فيها عطاءٌ فيستجيب لكم».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...
Kutoka kwa Jaabir bin Abdillah -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u:"Msiziombee mabaya nafsi nakhofia dua hizo zisikutane na muda ambao haombwi Mwenyezi Mungu katika muda huo chochote isipokuwa anakujibuni.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim]
Anatahadharisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi hii na anakataza kujiombea dua mbaya na kwa watoto na mali; kwasababu dua ni jambo kubwa, anaweza kuipitisha Mwenyezi Mungu kwa waja, ikiwa itaafikiana na saa ya kujibiwa ikawa madhara yake ni kwa mwenye nayo na yale yanayomuhusu kama watoto wake na mali yake.