+ -

عَن أَبِي أُمَامَةَ قَالَ: حَدَّثَنِي عَمْرُو بْنُ عَبَسَةَ رضي الله عنه أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«أَقْرَبُ مَا يَكُونُ الرَّبُّ مِنَ العَبْدِ فِي جَوْفِ اللَّيْلِ الآخِرِ، فَإِنْ اسْتَطَعْتَ أَنْ تَكُونَ مِمَّنْ يَذْكُرُ اللَّهَ فِي تِلْكَ السَّاعَةِ فَكُنْ».

[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي] - [سنن الترمذي: 3579]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Umama amesema: Alinisimulia Amru bin Abasa radhi za Allah ziwe juu yake kuwa, alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema:
"Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja ni katikati ya usiku wa mwisho, ikiwa utaweza kuwa miongoni mwa wanaomtaja Mwenyezi Mungu katika wakati huo basi fanya".

[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 3579]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mola Mtukufu yu karibu zaidi na mja katika theluthi ya mwisho ya usiku, ikiwa utawezeshwa na ukaweza - Ewe Muumini - kuwa miongoni mwa wanaoabudu, na kuswali, na kumtaja Mwenyezi Mungu na kutubia wakati huu, basi ni jambo ambalo unapaswa kulishika na kujitahidi.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية الرومانية Luqadda malgaashka
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Muislamu anahimizwa kumtaja Mwenyezi Mungu mwisho wa usiku.
  2. Nyakati zinazidiana ubora kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu na kuomba dua na kuswali.
  3. Amesema Muraik: Katika tofauti baina ya kusema kwake: “Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja,” na kusema kwake: “Mahala pa karibu zaidi anapokuwa mja na Mola wake Mlezi ni pale anapokuwa kasujudu”: Kinachokusudiwa hapa ni kuashiria wakati ambapo Mola anakuwa karibu zaidi na mja, yaani katikati ya usiku, na kinachokusudiwa hapo ni kueleza hali ya ukaribu wa mja na Mola ni pale anapokuwa katika hali ya kusujudu.