عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما قال: أقبَلَ رجل إلى نبي الله صلى الله عليه وسلم فقال: أُبَايِعُكَ على الهجرة والجهاد أَبْتَغِي الأجر من الله تعالى قال: «فَهَل لَكَ من وَالِدَيك أحد حيٌّ؟» قال: نعم، بل كلاهما، قال: «فتبتغي الأجر من الله تعالى؟» قال: نعم، قال: «فَارْجِع إلى وَالِدَيك، فَأَحْسِن صُحْبَتَهُمَا». وفي رواية لهما: جاء رجل إلى النبي صلى الله عليه وسلم فاستأذنه في الجهاد، فقال: «أَحَيٌّ والداك؟»، قال: نعم، قال: «فَفِيهِمَا فجاهد».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdillahi bin Amri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akasema: Nakupa mkono wa utiifu juu ya kuhama na jihadi nikitaraji malipo toka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, akasema: "Je kuna mmoja kati ya wazazi wako wawili yuko hai?" Akasema: Ndiyo, bali wote wawili, akasema: "Je unataka malipo toka kwa Allah?" Akasema: Naam, akasema: "Hebu rudi kwa wazazi wako, na ukaishi nao vizuri" Na katika riwaya nyingine ya kwao: alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akamuomba ruhusa ya kwenda jihadi, akasema: "Hivi wako hai wazazi wako?" Akasema: Ndiyo, akasema: "Basi kwao wao pigana jihadi". Kutoka kwa Abdillahi bin Amri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-akasema: Nakupa mkono wa utiifu juu ya kuhama na jihadi nikitaraji malipo toka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, akasema: "Je kuna mmoja kati ya wazazi wako wawili yuko hai?" Akasema: Ndiyo, bali wote wawili, akasema: "Je unataka malipo toka kwa Allah?" Akasema: Naam, akasema: "Hebu rudi kwa wazazi wako, na ukaishi nao vizuri" Na katika riwaya nyingine ya kwao: alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akamuomba ruhusa ya kwenda jihadi, akasema: "Hivi wako hai wazazi wako?" Akasema: Ndiyo, akasema: "Basi kwao wao pigana jihadi" Kutoka kwa Abdillahi bin Amri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akasema: Nakupa mkono wa utiifu juu ya kuhama na jihadi nikitaraji malipo toka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, akasema: "Je kuna mmoja kati ya wazazi wako wawili yuko hai?" Akasema: Ndiyo, bali wote wawili, akasema: "Je unataka malipo toka kwa Allah?" Akasema: Naam, akasema: "Hebu rudi kwa wazazi wako, na ukaishi nao vizuri" Na katika riwaya nyingine ya kwao: alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akamuomba ruhusa ya kwenda jihadi, akasema: "Hivi wako hai wazazi wako?" Akasema: Ndiyo, akasema: "Basi kwao wao pigana jihadi".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akimueleza kuhusu hamu yake na mapenzi yake ya jihadi na kuhama katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na alikuwa huyu bwana kaacha nyuma yake wazazi wake wawili, na imekuja katika riwaya ya Abuudaudi kuwa "Walikuwa wakilia", wakihofia maisha yake, akamuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Je kuna yeyote kati ya wazazi wako wawili yuko hai?" Akasema: Ndiyo, bali wote wawili, akasema: "Na unatafuta malipo toka kwa Allah?" Akasema: Ndiyo, akasema: "Basi rudi kwao ukawachekeshe kama ulivyowaliza". Akamrudisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika lile ambalo ni bora katika haki zake, nalo ni kurudi kwa wazazi wawili na aishi nao vizuri, kwani hilo ni katika kupambana na nafsi katika kusimamia kuwahudumia na kuwaridhisha na kuwatii, kama ilivyokuja katika riwaya ya Bukhariy na Muslim: "Basi kwao wao wawili pigana jihadi". Na aliweka wazi katika hadithi nyingine kuwa kuwafanyia wema wazazi wawili na kuwatii na kuwafanyia mazuri ni bora zaidi kuliko kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kama ilivyokuja katika riwaya nyingine ya kutoka kwa bin Omari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Anasema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akamuuliza kuhusu amali bora, akasema: "Ni swala" Akasema: kisha nini?: Akasema: "Jihadi" akasema: Hakika mimi nina wazazi wawili, akasema: "Kuwafanyia kwako wema wazazi wawili ndiyo bora" ameitoa bin Hibbaani, Imeonyesha hadithi hii kuwa kuwafanyia wema wazazi wawili ndiyo bora kuliko Jihadi, isipokuwa kama itakuwa Jihadi ni faradhi ya lazima, basi hapo itatangulizwa juu ya kuwatii wao; kwasababu ya ulazima wake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Kikurdi Kireno Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri
Kuonyesha Tarjama