عن ثوبان - رضي الله عنه- مولى رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: قَالَ رسولُ اللَّه -صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم-: «َأفضل دينار ينُفِقُهُ الرجل: دينار ينفقه على عياله، ودينار ينفقه على دَابَّتِهِ في سبيل الله، ودينار ينفقه على أصحابه في سبيل الله».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Thauban -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kijana wa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Dinari bora anayoitoa mtu: ni Dinari anayoitoa kwa familia yake, na Dinari anayoitoa kwa mnyama wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na Dinari anayoitoa kwa jamaa zake katika njia ya Mwenyezi Mungu".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Mali bora anazozitoa mtu katika njia za kheri, ni mali anayoitoa kwa familia yake, nao ni wale wote wanaomuhitajia, yaani: anaosimamia maisha yao kuanzia kwa mtoto wa kiume na wa kike na mke na mfanyakazi na wengineo, na mali anayoitoa kwa mnyama wake anayembeba katika mambo ya kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu kama Jihadi na mengineyo, na katika kauli nyingine nikuwa (katika njia ya Mwenyezi Mungu) maana yake ni Jihadi pekee.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kireno
Kuonyesha Tarjama