عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«كَلِمَتَانِ خَفِيفَتَانِ عَلَى اللِّسَانِ، ثَقِيلَتَانِ فِي الْمِيزَانِ، حَبِيبَتَانِ إِلَى الرَّحْمَنِ: سُبْحَانَ اللهِ الْعَظِيمِ، سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6406]
المزيــد ...
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Maneno mawili mepesi mno katika ulimi, ni mazito mno katika mizani, yanapendeka mno kwa Al-Rahmani (Mwingi wa rehema) Ni: Sub-haanallahil Adhwiim, Sub-haanallaahi wabihamdihi".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 6406]
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-kuhusu maneno mawili anayoyatamka mwanadamu bila uzito wowote na kwa hali yoyote, nakuwa maneno hayo malipo yake ni makubwa katika mizani, nakuwa Mola wetu Mlezi Mwingi wa rehema -Aliyetakasika na kutukuka- anayapenda:
Sub-haanallahil Adhwiim, Sub-haanallahi wabihamdihi; Kwakuwa yamekusanya sifa miongoni mwa sifa za Allah kumsifu kwa Utukufu na ukamilifu, na kumtakasa kutokana na mapungufu -Aliyetakasika na kutukuka-.