عَنْ عَبْدِ اللهِ بنِ مَسعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«عَلَيْكُمْ بِالصِّدْقِ، فَإِنَّ الصِّدْقَ يَهْدِي إِلَى الْبِرِّ، وَإِنَّ الْبِرَّ يَهْدِي إِلَى الْجَنَّةِ، وَمَا يَزَالُ الرَّجُلُ يَصْدُقُ وَيَتَحَرَّى الصِّدْقَ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللهِ صِدِّيقًا، وَإِيَّاكُمْ وَالْكَذِبَ، فَإِنَّ الْكَذِبَ يَهْدِي إِلَى الْفُجُورِ، وَإِنَّ الْفُجُورَ يَهْدِي إِلَى النَّارِ، وَمَا يَزَالُ الرَّجُلُ يَكْذِبُ وَيَتَحَرَّى الْكَذِبَ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللهِ كَذَّابًا».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2607]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
Kutoka kwa Abdillah bin Mas'udi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Shikamaneni na ukweli, kwani ukweli hupelekea katika wema, na hakika wema hupelekea katika pepo, na hatoacha mtu kuwa mkweli na akishughulika na ukweli mpaka ataandikwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni mkweli, na tahadharini na uongo, kwani uongo unapelekea katika uovu, na hakika uovu hupelekea katika moto, na hatoacha mtu kuendelea kuwa muongo, na akishughulika na uongo mpaka ataandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni muongo".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2607]
Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameamrisha ukweli, na akasema kuwa kushikamana nao kunapelekea katika matendo mema ya kudumu, na mwenye kushikamana na kufanya wema humpeleka mtendaji wake Peponi, na ukweli wake unapoendelea mara kwa mara kwa siri na hadharani, basi hustahiki jina la mkweli; nayo ni sifa ya hali ya juu zaidi ya ukweli. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaonya dhidi ya kusema uongo na kusema maneno ya batili; Kwa sababu inawachochea watu kuacha uadilifu, na kufanya maovu, ufisadi, na dhambi, kisha inawapeleka Motoni, na anapoendelea kukithirisha kusema uongo basi mpaka huandikwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni miongoni mwa waongo.