+ -

عَنْ شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«سَيِّدُ الِاسْتِغْفَارِ أَنْ تَقُولَ: اللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لاَ إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ، خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ، وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ، أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ، وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي فَاغْفِرْ لِي، فَإِنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ» قَالَ: «وَمَنْ قَالَهَا مِنَ النَّهَارِ مُوقِنًا بِهَا، فَمَاتَ مِنْ يَوْمِهِ قَبْلَ أَنْ يُمْسِيَ، فَهُوَ مِنْ أَهْلِ الجَنَّةِ، وَمَنْ قَالَهَا مِنَ اللَّيْلِ وَهُوَ مُوقِنٌ بِهَا، فَمَاتَ قَبْلَ أَنْ يُصْبِحَ، فَهُوَ مِنْ أَهْلِ الجَنَّةِ».

[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 6306]
المزيــد ...

Kutoka kwa Shadaad Bin Ausi Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Bwana wa Istighfari (Dua ya kuomba msamaha) Ni kusema: Allaahumma anta Rabbi Laa ilaaha illaa anta, khalaqtani wa anaa abduka wa ana a'laa a'hdika, wawa'dika mastatwa'tu, auudhubika min Sharri maa swana'tu, abuu ulaka bini'matika alaiyya, wa abuu ulaka bidhambi faghfirlii, fa innahuu laa yaghfirudh-dhunuuba illaa anta" Akasema: "Na atakayeisema dua hii mchana akiwa na yakini nayo, akafa katika mchana wake huo kabla hajafika jioni, basi atakuwa miongoni mwa watu wa peponi, na atakayeisema wakati wa usiku akiwa na yakini nayo, akafariki kabla hajafika asubuhi, basi huyo atakuwa miongoni mwa watu peponi".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 6306]

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaeleza kuwa Istighfari (Kuomba msamaha) kuna matamshi mengi, nakuwa matamshi bora na makubwa zaidi ni mja kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu wewe ndiye Mola Mlezi hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe, umeniumba na mimi ni mja wako na mimi nipo juu ya ahadi yako na maonyo yako kwa kiasi niwezavyo, ninataka hifadhi kwako kutokana na shari niliyo ifanya, ninakiri kwa neema zako zilizo juu yangu, na ninakiri kwa madhambi yangu, basi nisamehe mimi, kwani hakuna afutae madhambi isipokuwa wewe. Hivyo basi mja anaanza kukiri upweke wa Mwenyezi Mungu, nakuwa Mwenyezi Mungu ndiye muumba wake na muabudiwa wake hana mshirika wake, na kuwa yeye yuko katika ahadi aliyomuahidi Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, miongoni mwa imani na utiifu kwake, kwa kadiri ya uwezo wake; kwa sababu mja kwa namna yoyote atakavyotekeleza ibada hawezi kutekeleza yote aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu, na wala hawezi kutimiza haki stahiki katika kushukuru neema, nakuwa yeye anajilinda kwa Mwenyezi Mungu, na anajikinga kwake, kwani yeye ndiye mwenye kutakwa ulinzi kutokana na shari zote alizozitengeneza mja, Nakuwa yeye anakiri na kukubali kwa hiari yake neema zake juu yake, na anairudia nafsi yake kwa kukiri na kukubali madhambi yake na maasi yake, Na baada ya kupitia kwa Mwenyezi Mungu, atamuomba Mola wake asitiri makosa yake na amkinge na dhambi zake kwa msamaha wake na fadhila zake na rehema zake, kwani hakuna awezaye kusamehe madhambi ila yeye Mtukufu. Kisha akaeleza rehema na amani ziwe juu yake kuwa dua hii ni katika dhikiri na dua za asubuhi na jioni, nakuwa atakayeisema kwa yakini na kwa kuhudhurisha moyo wake na kwa kuiamini, mwanzo wa siku yake, kwanzia kuchomoza kwa Jua mpaka kupinduka kwake, nao ni wakati wa mchana, akafa, ataingia peponi, Na atakayeisema usiku, nao ni kuanzia kuzama kwa jua mpaka kuchomoza kwa Alfajiri, akafariki kabla hajafika asubuhi, ataingia peponi.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية التشيكية Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف الأوكرانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Namna za kuomba msamaha zinatofautiana na baadhi yake ni bora kuliko zingine.
  2. Nakuwa ni wajibu kwa mja apupie kumuomba Mwenyezi Mungu kwa dua hii; kwani ndio bwana wa dua zote za kuomba msamaha.