+ -

عَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه قَالَ:
كَانَ أَكْثَرُ دُعَاءِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «اللَّهُمَّ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً، وَفِي الآخِرَةِ حَسَنَةً، وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6389]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema:
Ilikuwa Dua aiombayo zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:ni "Ewe Mola wetu Mlezi, tupe duniani mazuri, na Akhera mazuri, na utukinge na adhabu ya moto".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 6389]

Ufafanuzi

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikithirisha dua kwa dua fupi zenye kukusanya mambo mengi, na miongoni mwake: "Ewe Mwenyezi Mungu! Tupe hapa katika Dunia (mambo) mazuri, na Akhera utupe mazuri na utukinge na adhabu ya moto", Dua hii inakusanya mazuri yote ya Dunia; ikiwemo riziki ya raha na pana na ya halali, na mke mwema, na mtoto kitulizo cha jicho, na starehe, na elimu yenye manufaa, na mfano wa hayo miongoni mwa maombi yanayopendeka na ya halali, na mazuri ya Akhera ni kusalimika na adhabu za kaburi, na kisimamo cha Kiyama na moto, na kupata radhi za Mwenyezi Mungu, na kufaulu kwa kupata neema za kudumu, na kuwekwa karibu na Mola Mlezi Mwingi wa huruma.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية التشيكية Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Sunna ya kuomba dua kupitia dua zinazokusanya maana pana, kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  2. Kwa ukamilifu zaidi ni mtu akusanye katika maombi yake baina ya kheri za Dunia na Akhera.