عَنْ سَلْمَانَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِنَّ رَبَّكُمْ حَيِيٌّ كَرِيمٌ، يَسْتَحْيِي مِنْ عَبْدِهِ إِذَا رَفَعَ يَدَيْهِ إِلَيْهِ أَنْ يَرُدَّهُمَا صِفْرًا».
[حسن] - [رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه] - [سنن أبي داود: 1488]
المزيــد ...
Na kutoka kwa Salmani -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye haya Mkarimu, anamuonea haya mja wake atakapo nyanyua mikono yake kumuelekezea kisha amrejeshe patupu".
[Ni nzuri] - - [سنن أبي داود - 1488]
Anahimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kunyanyua mikono wakati wa dua, na akaeleza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu "huona haya" mwingi wa haya, na haachi kutoa, anamfanyia mja yenye kumfurahisha, na anaacha yenye kumdhuru, "Ni Mkarim" hutoa pasina kuombwa, je hali huwaje baada ya kuombwa! anamuonea haya mja wake muumini kuirejesha patupu mikono yake baada ya kuinyanyua kwa ajili ya dua ikiwa imefeli haina kitu kwa kutojibiwa.