+ -

عَنْ عِيَاضِ بْنِ حِمَارٍ أَخِي بَنِي مُجَاشِعٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَامَ فِينَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ذَاتَ يَوْمٍ خَطِيبًا، فَقَالَ: وَسَاقَ الْحَدِيثَ وَفِيهِ:
«وَإِنَّ اللهَ أَوْحَى إِلَيَّ أَنْ تَوَاضَعُوا حَتَّى لَا يَفْخَرَ أَحَدٌ عَلَى أَحَدٍ، وَلَا يَبْغِي أَحَدٌ عَلَى أَحَدٍ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2865]
المزيــد ...

Kutoka kwa Iyaadh bin Himari ndugu yao na Bani Mujashii radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alisimama kwetu Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake siku moja kwa ajili ya kuhutubia, akasema: Na akaeileza hadithi na ndani yake alisema:
"Na hakika Mwenyezi Mungu ameniteremshia wahyi kuwa, kuweni wanyenyevu, mpaka asijikweze yeyote kwa mwingine, na wala asimfanyie uadui yeyote mwenzake"

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2865]

Ufafanuzi

Alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Maswahaba zake wakati akihutubia, na ikawa miongoni mwa yale aliyosema ni: Hakika Mwenyezi Mungu amemteremshia wahyi ya kwamba ni wajibu kwa watu wanyenyekeane wao kwa wao, na hii ni kwa kushusha mbawa (kujishusha) kwa viumbe na kuwa wapole, mpaka asijikweze kwa kudai ukubwa na kiburi na utukufu yeyote kwa ukoo wake au mali yake au kinginecho juu ya yeyote, na wala asidhulumu na asifanye uadui yeyote kwa mwenzake.

Katika Faida za Hadithi

  1. Katika hadithi kuna himizo la kuwa wanyenyekevu na kutokuwa na kiburi na kujikweza juu ya watu.
  2. Katazo la uadui na ufahari.
  3. Kujinyenyekeza kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kuna maana mbili: Maana ya kwanza: Ni mtu unyenyekee kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu, usijikweze katika dini, na wala usiwe na kiburi, na kutekeleza hukumu zake. Na ya pili: Ni unyenyekee kwa waja wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, si kwa sababu ya kuwaogopa, na wala si kwa kutaraji walivyonavyo, lakini ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama