+ -

عن النعمان بن بَشِير رضي الله عنه قال: سمعت النبيَّ صلى الله عليه وسلم يقول:
«الدُّعَاءُ هُوَ الْعِبَادَةُ»، ثُمَّ قَرَأَ: «{وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ} [غافر: 60]».

[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه وأحمد] - [سنن الترمذي: 3247]
المزيــد ...

Imepokewa Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Dua ndio ibada", Kisha akasoma: "Na amesema Mola wenu Mlezi niombeni mimi nitakujibuni, hakika wale wanaofanya kiburi katika ibada yangu wataingia Jahannam wakiwa madhalili" [Ghafir: 60].

[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 3247]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa dua ndio ibada, la msingi nikuwa yote iwe safi kwa ajili ya Allah, sawa sawa iwe ni kuomba jambo au kutaka jambo, kwa kumuuomba Allah Mtukufu ampe yenye manufaa kwake, na amkinge na yenye kumdhuru duniani na akhera, au dua ikiwa ni ibada, nayo ni kila anayoyapenda Mwenyezi Mungu na kuyaridhia katika kauli na matendo ya wazi na ya siri, ibada za moyo au za mwili au za mali.
Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akatoa ushahidi juu ya hilo pale aliposema: Amesema Allah Mtukufu: "..Niombeni mimi nitakujibuni, hakika wale wanaofanya kiburi katika ibada yangu wataingia Jahannam wakiwa madhalili"

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka الفولانية Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga الأوزبكية الأوكرانية الجورجية اللينجالا المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Dua ndio asili ya ibada na wala haifai kuilekeza kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
  2. Dua inaambatana na uhalisia wa kuabudu na kukiri utajiri wa Mola Mlezi na uwezo wake Yeye Mtukufu, na uhitaji wa mja kwake.
  3. Kemeo kali likiwa ni malipo ya kiburi cha kutomuabudu Mwenyezi Mungu na kuacha kumuomba, nakwamba wale wanaofanya jeuri kumuomba Allah wataingia katika Jahannam wakiwa wanyonge madhalili.