عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعاً: «ليس شيءٌ أكرمَ على الله من الدعاء».
[حسن] - [رواه الترمذي وابن ماجه وأحمد]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Hakuna kitu kitukufu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko dua".
Ni nzuri - Imepokelewa na Ibnu Maajah

Ufafanuzi

(Hakuna kitu kitukufu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko dua) kwakuwa ni ibada, na ibada ni ile ambayo amewaumba Mwenyezi Mungu Mtukufu viumbe kwaajili yake, dua inaonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu na upana wa elimu yake, na udhaifu wa muombaji na uhitaji wake, kwaajili hii dua ikawa ni katika vitu vitukufu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Ubora wa dua nakuwa ni kitu bora na kitukufu kuliko vitu vyote kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  2. Kuhimizwa juu ya dua, na kuipupia, kwakuwa ni kitu kitukufu zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.