عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَا جَلَسَ قَوْمٌ مَجْلِسًا لَمْ يَذْكُرُوا اللَّهَ فِيهِ وَلَمْ يُصَلُّوا عَلَى نَبِيِّهِمْ إِلاَّ كَانَ عَلَيْهِمْ تِرَةً، فَإِنْ شَاءَ عَذَّبَهُمْ وَإِنْ شَاءَ غَفَرَ لَهُمْ».
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي في الكبرى] - [سنن الترمذي: 3380]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Hawajawahi kukaa watu kikao chochote wakawa hawakumtaja Mwenyezi Mungu ndani yake, na wala hawakumsalia Nabii wao, isipokuwa itakuwa ni hasara juu yao, akitaka atawaadhibu na akitaka atawasamehe".
[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 3380]
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kughafilika kumtaja Mwenyezi Mungu, nakuwa hawatokaa watu katika kikao chochote na wakawa hawakumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, na wakawa hawakumsalia Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake isipokuwa kikao hicho kitakuwa ni hasara na majuto juu yao na mapungufu siku ya Kiyama, akitaka atawaadhibu kwa madhambi yao yaliyotangulia na uzembe wao uliofuata, na akitaka atawasamehe ikiwa ni fadhila na rehema kutoka kwake.