عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ رضي الله عنه: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«إِنَّ اللَّعَّانِينَ لَا يَكُونُونَ شُهَدَاءَ وَلَا شُفَعَاءَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2598]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abud-dardaa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema:
"Hakika watoa laana hawatokuwa mashahidi wala watetezi siku ya Kiyama".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2598]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kukithirisha laana kwa mtu asiyestahiki huyu anastahiki kupata adhabu mbili. Ya kwanza: Hatokuwa shahidi siku ya Kiyama juu ya umma kwa mitume wao kufikisha ujumbe kwao, na wala haukubaliki ushahidi wake duniani; kwa sababu ya uovu wake, na wala hatoruzukiwa shahada, nako ni kufa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Ya pili: Hatopewa nafasi ya kutoa utetezi siku ya Kiyama wakati ambapo waumini wataomba utetezi kwa ndugu zao waliostahiki moto.