+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«الْمُؤْمِنُ الْقَوِيُّ، خَيْرٌ وَأَحَبُّ إِلَى اللهِ مِنَ الْمُؤْمِنِ الضَّعِيفِ، وَفِي كُلٍّ خَيْرٌ، احْرِصْ عَلَى مَا يَنْفَعُكَ، وَاسْتَعِنْ بِاللهِ وَلَا تَعْجَزْ، وَإِنْ أَصَابَكَ شَيْءٌ، فَلَا تَقُلْ لَوْ أَنِّي فَعَلْتُ كَانَ كَذَا وَكَذَا، وَلَكِنْ قُلْ قَدَرُ اللهِ وَمَا شَاءَ فَعَلَ، فَإِنَّ (لَوْ) تَفْتَحُ عَمَلَ الشَّيْطَانِ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2664]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, na katika kila kheri, Pupia yenye manufaa na wewe, na utake msaada kwa Allah na wala usishindwe, na likikusibu jambo usiseme: Lau ningelifanya kadha basi ingelikuwa kadhaa wa kadhaa, lakini sema: Hili ni kwa makadirio ya Allah naye hufanya alitakalo, maana neno "Lau" hufungua matendo ya shetani".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2664]

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muumini ni mtu wa kheri maisha yake yote, lakini muumini mwenye nguvu katika imani yake na maamuzi yake na mali yake na mengineyo yenye kuendana na nguvu huyu ni bora zaidi na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko muumini dhaifu. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuusia muumini kuchukuwa sababu katika yale yenye kumnufaisha katika mambo ya Dunia na Akhera, ikiwa ni pamoja kuegemea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutaka msaada kwake, na kutegemea kwake. Kisha akakataza rehema na amani ziwe juu yake kuhusu kushindwa, na uvivu, na uzembe wa mtu kufanya yale yenye manufaa Duniani na Akhera. Muumini akijitahidi katika matendo, na akachukua sababu, huku akitaka msaada kwa Mwenyezi Mungu, na kwa kutaka kheri kutoka kwa Mwenyezi Mungu, basi hapo hana la kufanya zaidi ya kukabidhi jambo lake lote kwa Mwenyezi Mungu, na ajue kuwa uchaguzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndio wenye kheri, ukimpata msiba baada ya hapo, basi asiseme: "Laiti ningelifanya kadha wa kadha"; "Kwani neno "Lau" Hufungua kazi ya Shetani" kuanzia kupingana na mipango ya Allah, na kuhuzunika kwa yale aliyoyakosa, bali anatakiwa aseme tena kwa kujisalimisha na kuridhika: "Ni mipango ya Mwenyezi Mungu na alitakalo hufanya", kilichotokea ni kwa mujibu wa yale aliyoyataka Mwenyezi Mungu, kwani yeye ni mfanyaji asiye na mipaka wa yale ayatakayo, na hakuna awezaye kuzuia maamuzi yake, na hakuna awezaye kuhukumu baada ya hukumu yake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية التشيكية Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف الأوكرانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kutofauti watu katika swala la imani.
  2. Inapendeza kuwa na nguvu katika matendo; kwani hupatikana faida kwa matendo hayo ambayo haipatikani kukiwa na udhaifu.
  3. Mwanadamu anatakiwa apupie katika yale yenye kumnufaisha, na aache yasiyomnufaisha.
  4. Ni wajibu kwa muumini atake msaada wa Mwenyezi Mungu kwake katika mambo yake yote, na wala asiitegemee nafsi yake.
  5. Kuthibiti uwepo wa mipango na maamuzi ya Mwenyezi Mungu (kadhaa na kadari), nakuwa hilo halipingani na swala la mtu kufanya sababu na kwenda kutafuta mambo mazuri na ya kheri.
  6. Katazo la kusema: "Lau" kwa njia ya kulalamika wakati wa kupatwa na mitihani, na uharamu wa kupingana na maamuzi na mipango ya Allah Mtukufu.