عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ إِذَا أَصْبَحَ: «اللهُمَّ بِكَ أَصْبَحْنَا، وَبِكَ أَمْسَيْنَا، وَبِكَ نَحْيَا، وَبِكَ نَمُوتُ، وَإِلَيْكَ النُّشُورُ» وَإِذَا أَمْسَى قَالَ: «بِكَ أَمْسَيْنَا، وَبِكَ أَصْبَحْنَا، وَبِكَ نَحْيَا، وَبِكَ نَمُوتُ، وَإِلَيْكَ النُّشُورُ» قَالَ: وَمَرَّةً أُخْرَى: «وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ».
[حسن] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي في الكبرى وابن ماجه] - [السنن الكبرى للنسائي: 10323]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
Yakwamba yeye alikuwa akisema anapoamka: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka, na kwako tunashinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutakufa, na kwako tutafufuliwa" Na anaposhinda jioni anasema: "Kwako tumeshinda, na kwako tumeamka, na kwako tunakuwa hai, na kwako tunakufa, na kwako tutafufuliwa" Akasema: Na mara nyingine: "Na kwako ndio marejeo".
[Ni nzuri] - - [السنن الكبرى للنسائي - 10323]
Alikuwa rehema na amani ziwe juu yake anapofikiwa na asubuhi nayo ni mwanzo wa mchana pamoja na kuchomoza Alfajiri anasema:
"Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka" tukiwa tumegubikwa na hifadhi yako na kufunikwa na neema zako, tukishughulika na kukutaja, tukitaka msaada kwa jina lako, tukienewa na taufiki yako, tukifanya harakati zenu kwa ujanja wako na nguvu zako, "na kwako tumeshinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tunakufa" yaani; hii ni kama lafudhi iliyotangulia isipokuwa hii imefanywa ya jioni, atasema: Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeshinda, na kwa jina lako Muhuishaji tunakuwa hai, na kwa jina lako Mfishaji tutakufa, "na kwako tutafufuliwa" na kufufuliwa baada ya kifo, na kusambaa baada ya kukusanywa, itaendelea hali yetu namna hii katika nyakati zote, na hali zingine zilizobakia, na wala sitoachana nayo wala sitoihama.
Na ikimfikia jioni baada ya Lasiri atasema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeshinda, na kwako tumeamka, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutafuka, na marejeo ni kwako" na marejeo katika dunia, na mafikio katika mwisho, wewe ndiye unayenihuisha na wewe ndiye unayenifisha.