عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«مَنْ يُرِدِ اللهُ بِهِ خَيْرًا يُصِبْ مِنْهُ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 5645]
المزيــد ...
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Mwenye kutakiwa kheri na Allah, (Allah) humuonja kutokana na kheri hiyo.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح ابن حبان - 5645]
Anaeleza Mtume -Rehama na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu akitaka kheri kwa yeyote katika waja wake waumini huwapa mtihani katika nafsi zao na mali zao, na familia zao, kwa kile kinachotokea kwa muumini ikiwemo kurejea kwa Allah Mtukufu kwa maombi na dua, na kufutiwa makosa, na kunyanyuliwa daraja.