عن البراء بن عازب رضي الله عنه مرفوعاً: «المسلمُ إذا سُئِلَ في القَبْرِ يَشْهَدُ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ، وأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ، فذلك قولُهُ تعالى: (يُثَبِّتُ اللهُ الذِينَ آمَنُوا بالقَوْلِ الثَّابِتِ في الحَيَاةِ الدُّنْيَا وفي الآخِرَةِ) [إبراهيم: 27]».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
kutoka kwa Albaraa bin Aazib Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Muislamu atakapoulizwa kaburini anashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu", Hiyo ndiyo kauli yake Mtukufu: "Huwapa umakinifu Mwenyezi Mungu wale walioamani kwa kauli thabiti katika maisha ya dunia na katika akhera" [Ibrahim: 27].
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Muumini ataulizwa kaburini, watamuuliza Malaika wawili waliopangiwa kufanya hivyo, nao ni Munkari na Nakiri, kama walivyotajwa katika Hadithi kadhaa, atashuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hii ndio kauli thabiti aliyoisema Mwenyezi Mungu: "Huwapa umakinifu Mwenyezi Mungu wale walioamani kwa kauli thabiti katika maisha ya dunia na katika akhera" [Surat Ibrahim: 27].