عن خَوْلَةَ بِنْتَ حَكِيمٍ السُّلَمِيَّةَ قَالتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«مَنْ نَزَلَ مَنْزِلًا ثُمَّ قَالَ: أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ، لَمْ يَضُرَّهُ شَيْءٌ حَتَّى يَرْتَحِلَ مِنْ مَنْزِلِهِ ذَلِكَ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2708]
المزيــد ...
Kutoka kwa Khaula bint Hakim As-Sulamiyya, amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Atakayeshuka mahali akasema: Audhubikalimaatillaahit-taammaati min sharri maa khalaqa (Najilinda kwa maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyotimia kutokana na shari ya vile alivyoviumba) hakitomdhuru kitu mpaka aondoke mahala pake hapo".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2708]
Anauelekeza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake katika kushikamana na kukimbilia kwenye tija ambako hutoeka kila chenye kuogofya anachokiogopa mwanadamu pale anaposhuka mahali katika ardhi, sawa sawa awe safarini au matembezini na kwingineko: Kuwa ajikabidhi na atake ulinzi kupitia maneno ya Allah yaliyotimia katika fadhila zake na baraka zake na manufaa yake, yaliyosalimika na kila aibu na mapungufu, kutokana na shari ya kila kiumbe chenye shari, ili awe na amani katika mazingira yake hayo kwa muda wote atakaokuwa hapo kutokana na kila chenye kuudhi.