عَنْ جَابِرٍ رَضيَ اللهُ عنهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَنْ قَالَ: سُبْحَانَ اللهِ العَظِيمِ وَبِحَمْدِهِ، غُرِسَتْ لَهُ نَخْلَةٌ فِي الجَنَّةِ».
[صحيح] - [رواه الترمذي] - [سنن الترمذي: 3464]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakayesema: Sub-haanallaahi wabihamdi, (Ametakasika Mwenyezi Mungu Mtukufu na sifa njema ni zake) ataoteshewa mti wa mtende peponi".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy] - [سنن الترمذي - 3464]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa atakayesema: "Ametakasika Mwenyezi Mungu" ninamtakasa "Mtukufu" kwa dhati yake na sifa zake na vitendo vyake "na sifa njema ni zake" zikiwa zimeambatanishwa na kuegemeza sifa za ukamilifu wake Mtukufu; atasimikiwa na kupandiwa mti wa mtende katika ardhi ya Pepo kwa kila mara atakayosema.