عن أبي موسى الأشعري - رضي الله عنه- قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «من صلى البَرْدَيْنِ دخل الجنة».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Musa Al Ash'ariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: Amesema Mtume Rehema na Amani zimfikie: "Atakayeswali (katika nyakati mbili) za baridi mbili ataingia peponi".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Maana ya hadithi hii: nikuwa kuzihifadhi swala hizi mbili ni katika sababu za kuingia peponi. Na makusudio ya swala hizo mbili ni: swala ya Alfajiri na swala ya Laasiri, na kinachoonyesha hivyo ni kauli yake Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi ya Jariir: "Ni swala kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuzama kwake" Akaongeza katika riwaya ya Muslim yaani:"Ni Laasiri na Alfajiri" kisha akasoma Jariir: (Na umtukuze Mola wako kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuzama kwake). Na zimeitwa kuwa "za baridi mbili"; kwasababu huswaliwa nyakati za baridi ya mchana nazo ni mwanzo wake, wakati upepo unapokuwa safi na ukaondoka ukali wa joto. Na zimekuja hadithi nyingi zikionyesha ubora wa swala hizi mbili, na miongoni mwazo ni ile iliyopokelewa na Ammara bin Ruayba kutoka kwa baba yake kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- (Hatoingia motoni mtu aliyeswali kabla ya kuchomoza jua na kabla halijazama) kaipokea Muslim (634). Na sababu ya kuzitenga hizi mbili katika kuzitaja nikuwa wakati wa Alfajiri huwa ni wakati wa kulala na ladha yake, na wakati wa Laasiri hua ni wakati wa shughuli za kuhitimisha kazi za mchana na biashara zake, katika kuziswali kwake swala hizo mbili pamoja nakuwa ni ushahidi wa kuwa nafsi imeepukana na uvivu na kupenda kwake ibada, na inapelekea hiyo kutekeleza swala zingine zote, nakuwa yeye atakapozidumisha basi zingine atazidumisha zaidi, hivyo kutajwa pekee wakati zilipotajwa haimaanishi kuwa atakayetosheka na hizo; kwa kuzileta hizo tu bila zingine atapata malipo hayo (pepo); kwasababu hilo liko kinyume na ushahidi. Na kauli yake -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Atakayeswali (nyakati) za baridi mbili" Makusudio yake nikuwa aziswali kwa namna aliyoamrishwa, hiyo ni pamoja na kuziswali kwa wakati wake, na atakapokuwa ni katika watu wanaolazimika kuziswali kwa jamaa (msikitini) kama wanaume basi aziswali pamoja na jamaa; kwasababu jamaa ni wajibu, na wala haitakiwi kwa mwanaume kuiacha jamaa msikitini hali yakuwa anaweza.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno الدرية
Kuonyesha Tarjama