عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعاً: «من صَام رمضان إيِمَانًا واحْتِسَابًا، غُفِر له ما تَقدَّم من ذَنْبِه».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Hadithi Marfu'u: "Atakayefunga ramadhani kwa imani na kwa kutaraji malipo, atasamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Maana ya hadithi: Nikuwa atakayefunga mwezi wa ramadhani kwa kumuamini Mwenyezi Mungu na kwa kusadikisha ahadi zake na kwa kutaraji malipo yake na kwa kukusudia radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, si kwa kujionyesha wala kutaka kusikika, atasamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kubainishwa ubora wa ramadhani na utukufu wa heshima yake, nakuwa ni mwezi wa kufunga, atakayeufunga yatasamehewa makosa yake na madhambi yake hata kama yalikuwa kama povu la bahari.
  2. Kunafaa kusema ramadhani bila kuongeza neno mwezi.