عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«قَالَ اللَّهُ: كُلُّ عَمَلِ ابْنِ آدَمَ لَهُ، إِلَّا الصِّيَامَ، فَإِنَّهُ لِي وَأَنَا أَجْزِي بِهِ، وَالصِّيَامُ جُنَّةٌ، وَإِذَا كَانَ يَوْمُ صَوْمِ أَحَدِكُمْ فَلاَ يَرْفُثْ وَلاَ يَصْخَبْ، فَإِنْ سَابَّهُ أَحَدٌ أَوْ قَاتَلَهُ، فَلْيَقُلْ إِنِّي امْرُؤٌ صَائِمٌ، وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ، لَخُلُوفُ فَمِ الصَّائِمِ أَطْيَبُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ رِيحِ المِسْكِ، لِلصَّائِمِ فَرْحَتَانِ يَفْرَحُهُمَا: إِذَا أَفْطَرَ فَرِحَ، وَإِذَا لَقِيَ رَبَّهُ فَرِحَ بِصَوْمِهِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1904]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Amesema Mwenyezi Mungu: Kila amali ya mwanadamu hiyo ni ya kwake isipokuwa swaumu, bila shaka hiyo ni yangu na mimi ndiye ninayeilipa, na swaumu ni kinga, na itakapokuwa ni siku ya kufunga mmoja wenu basi asitamke machafu, wala asifanye fujo, na ikiwa kuna mtu atamtukana au akampiga, basi aseme, mimi nimefunga, namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hakika harufu ya mdomo wa mfungaji ni nzuri mno mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko harufu ya Miski, mfungaji anafuraha mbili anazofurahia: Anapofuturu hufurahi, na akikutana na Mola wake atafurahi kwa swaumu yake"
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1904]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika hadithil Kudsi kuwa:
Amali zote za mwanadam mema huzidishwa jema moja kwa mara kumi mfano wake mpaka ziada mia saba, isipokuwa swaumu; kwani hiyo ni yangu kiasi kwamba huwa haifikiwi na ria, na mimi ndiye ninayeilipa, hivyo ninabaki peke yangu katika kujua kiwango cha thawabu zake na uzidishwaji wa mema yake.
Kisha akasema: "Na swaumu ni kinga" Ni kinga na ni ngome madhubuti dhidi ya moto; kwa sababu ni kujizuia na matamanio na kutumbukia katika madhambi, na moto umezingirwa na matamanio.
"Itakapokuwa ni siku ya kufunga kwa mmoja wenu basi asifanye machafu" kwa tendo la ndoa na vitangulizi vyake, wala kwa maneno machafu moja kwa moja.
"Wala asifanye fujo" Kwa ugomvi na zogo.
"Na ikiwa mtu atamtukana au kumpiga" Katika mwezi wa Ramadhani basi na aseme: Mimi ni mtu niliyefunga; huenda akamuacha, ikiwa ataendelea na kukawa hakuna namna zaidi ya kupigana naye pasina utani basi na amsukume kidogo kidogo kama anamtenza nguvu.
Kisha akaapa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na akamuapia yule ambaye nafsi yake iko mkononi mwake kuwa kubadilika kwa harufu ya kinywa cha mfungaji kwa sababu ya swaumu hiyo ni nzuri mno mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama kuliko harufu ya Misiki kwenu, na inamalipo mengi kuliko Miski iliyohimizwa katika swala za Ijumaa na vikao vya kumtaja Mwenyezi Mungu.
Na mfungaji anafuraha mbili anazofurahia: Anapofungua anafurahia kufungua kwake kwa kuondoka njaa yake na kiu yake kwa kuhalalishiwa kufungua, na anafurahi kwa kutimia swaumu yake na kufikia kikomo kwa ibada yake, na wepesi kutoka kwa Mola wake Mlezi, na nimsaada kwa mustakabali wa swaumu yake.
"Na akikutana na Mola wake Mlezi atafurahi kwa swaumu yake" Kwa malipo yake na thawabu zake.