عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِذَا لَقِيَ أَحَدُكُمْ أَخَاهُ فَلْيُسَلِّمْ عَلَيْهِ، فَإِنْ حَالَتْ بَيْنَهُمَا شَجَرَةٌ أَوْ جِدَارٌ أَوْ حَجَرٌ ثُمَّ لَقِيَهُ فَلْيُسَلِّمْ عَلَيْهِ أَيْضًا».
[صحيح] - [رواه أبو داود] - [سنن أبي داود: 5200]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakapokutana mmoja wenu na ndugu yake basi na amsalimie, ukiwatenganisha kati yao mti, au ukuta, au jiwe, kisha akakutana naye tena basi amsalimie tena"
[Sahihi] - [Imepokelewa na Abuu Daud] - [سنن أبي داود - 5200]
Mtume rehema na amani ziwe juu yake anamhimiza muislamu kumsalimia ndugu yake muislamu kila anapokutana naye, hata kama wakiwa wanatembea pamoja na kikawatenganisha chochote, kama mti au ukuta au jiwe kubwa, kisha akakutana naye baada ya hapo basi amsalimie kwa mara nyingine.