عن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«إِذَا مَرِضَ الْعَبْدُ أَوْ سَافَرَ كُتِبَ لَهُ مِثْلُ مَا كَانَ يَعْمَلُ مُقِيمًا صَحِيحًا».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 2996]
المزيــد ...
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ariy -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Pindi anapougua mja au akasafiri basi huandikiwa mfano wa yale aliyokuwa akiyafanya akiwa nyumbani tena mwenye afya".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 2996]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu fadhila za Allah na rehema zake, nakuwa muislamu ikiwa ni katika mazoea yake kufanya matendo mema akiwa katika hali ya afya na yuko nyumbani, kisha apatwa na udhuru akaugua akashindwa kutekeleza ibada hizo, au akashughulishwa na safari, au udhuru wowote; basi huandikiwa malipo kamili, kama ambavyo angefanya wakati wa afya na yuko nyumbani.